TCRA YAKUTANA NA WATOA HUDUMA NA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA

Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imekutana na Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.

Mkutano huo uliopewa jina la ‘Consumer Forum’ umefanyika leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Buzuruga Jijini Mwanza.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo amewataka watumiaji wa huduma za mawasiliano kufanya uhakiki wa usajili wa laini ya simu kwa kupiga *106#, kutumia namba 100 kwa ajili ya huduma kwa mteja na kutumia namba 15040 endapo watapigiwa simu au kupata ujumbe wa kitapeli.

“Ili kuhakiki namba zako za simu zilizosajiliwa kwa namba ya kitambulisho chako cha NIDA piga *106# na kama utabaini kuna namba zipo lakini hujazisajili toa taarifa kwa mtoa huduma wako wa huduma za mawasiliano ili wazuie namba hizo”,amesema Ringo.

“Siyo kila simu au SMS inayoingia kwenye simu yako ni halali. Tumia namba 15040 (Tuma neno Utapeli) endapo utapigiwa simu au kupata ujumbe wa kitapeli, sisi tutaifanyia kazi. Usitume pesa kwa mtu usiyemfahamu, hakiki Ujumbe na namba inayokutaka utume pesa kabla ya kufanya muamala na kumbuka Mawasiliano baina ya mteja wa huduma za mawasiliano ya simu na mtoa huduma wake ni kuptia namba 100 pekee”, ameongeza Ringo.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi  hususani vijana kutumia mitandao ya kijamii 'Intaneti' kwa ajili ya maendeleo na kuachana na tabia ya kutuma picha chafu mtandaoni ili kukabiliana na mmonyoko wa maadili katika jamii.

Nao Watumiaji wa huduma za mawasiliano , wameeleza baadhi ya malalamiko yao kuwa ni pamoja na namba ya huduma kwa mteja namba 100 kwenye kampuni za simu kuchukua muda mrefu kupokelewa, gharama ya vifurushi (Bando) kuwa juu na kuisha haraka, Laini za simu kufutwa bila mtumiaji kupewa taarifa wakisema ni bora watoa huduma za mawasiliano wangekuwa wanaziondoa tu hizo laini kwenye mfumo badala ya kumpatia mtu mwingine hali inayosababisha taarifa za mtumiaji wa awali kupelekwa kwa mtumiaji mwingine.
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo  akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano leo Ijumaa Novemba 25,2022 katika ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza

Meneja wa Sehemu ya Wateja na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo akiongoza Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.

Afisa Mkuu wa TEHAMA TCRA, Irene Kahmili akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.

Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji wa huduma za mawasiliano mkoa wa Mwanza, Jonathan Kassibu akizungumza kwenye Mkutano wa Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kukuza Sekta ya Mawasiliano.

Watoa Huduma za Mawasiliano na Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post