HAKUNA MBABE...YANGA NA SIMBA WATOSHANA NGUVU KWA MKAPA

WAKIWA wenyeji wa Mchezo Mabingwa watetezi Yanga wameshindwa kutamba mbele ya Simba baada ya kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC iliyochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Mchezo wa watani wa Jadi uliosimamisha nchi kwa dakika 90 uliohudhuriwa na wadau wa mchezo mashabiki wa timu zote mbili uwanja wakipambwa na jezi za Njano,Kijana na Nyekundu na Nyeupe.


Simba walianza kupata bao kupitia kwa winga wao hatari Augustine Okrah dakika ya 15 akimalizia pasi Clatous Chama huku Yanga wakipata bao kupitia kwa Kiungo Mshambuliaji wao Stephanie Aziz Ki dakika ya 45 baada ya kupiga Mpira wa faulo ulioenda moja kwa moja.


Kipindi cha Pili timu zote zilifanya mabadiliko huku kosakosa zikiendelea kila upande hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho hakuna aliyeweza kuondoka na pointi tatu.


Kwa matokeo hayo Simba wanaendelea kukaa kileleni wakiwa na Pointi 14 sawa na Yanga wenye Pointi hizo 14 huku Simba akifaidika na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments