AJIGAMBA ANAVYONUSA NGUO ZA NDANI ZA MMEWE KUBAINI MICHEPUKO

Mwanamitindo na mfanyabiashara Kimberly Flores, amefunguka na kudai kwamba ana mazoea ya kunusa chupi/boxer za mumewe mwimbaji Edwin Luna, kubaini iwapo ana uhusiano nje ya ndoa.

Mwanamitindo huyo wa Guatemala, alidai aliamua kuchukua hatua hiyo, katika juhudi za kuhakikisha mumewe anasalia mwaminifu kwake.

Kimberley alidao kwamba kunusa chupi za mumewe kutaka ushahidi iwapo ana mpango wa kando. 

Na sio hayo tu, Kimberley alisema kwamba yeye hupitia ukurasa rasmi wa Instagram unaomilikiwa na mumewe, ili kupitia jumbe kuona iwapo kuna mwanamke anayeweza kutishia ndoa yao.

Pia, yeye huangalia iwapo ametumia pesa zake kwa wanawake wengine.

 “Mimi huangalia iwapo ametumia credit card kuwanunulia watu wengine vitu, niangalie pia amempigia simu nani usiku wa manane, na hata kunusa chupi zake. . . na kufuatilia mitandao yake ya kijamii kama vile Instagram,” Kimberley alisema.

 Mwanamitindo huyo alisema kwamba kufikia sasa, mumewe ni mwaminifu.

Video hiyo ilizua hisia mseto huku wengine wakiona tabia yake Kimberley ya kunusa chupi, kuwa ni upuuzi wa kutaka kumthibiti mumewe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post