NAIBU WAZIRI WA MAJI AONYA WANAOCHEPUSHA MAJI


Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na wananchi wa kijiji cha Mpanga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Oktoba 27, 2022.

Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akicheza na wananchi wa kijiji cha Mpanga katika halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe waliokuwa wakifurahia kijiji chao kubaki kwenye eneo la hifadhi ya Pori la Akiba la Mpanga Kipengele wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ilipofanya ziara katika mkoa wa Njombe Oktoba 27, 2022.

Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akiwa na Mawaziri wenzake wa wizara za kisekta wakati wa mkutano wa hadhara kwenye kijiji Mpanga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Oktoba 27, 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

**********************

Na Munir Shemweta, WANMM WANGING’OMBE

Meryprica mahindi ameonya wale wote wanaochepusha maji kwa ajili ya kufanya shughuli zao ikiwemo kumwagia mashamba na kueleza kuwa, kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

Meryprica alisema hayo Oktoba 27, 2022 wakati kamati ua mawaziri nane wa wizara za kisekta kushughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi ilipokwenda kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mpanga katika halmashauri ya wilaya ya Wanging,'ombe mkoani Njombe.

Aliwataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza maeneo maji yanapoanzia na kufuata sheria pale wanapotaka kutumia na kusisitiza wanaochepusha maji kiholea waache kuacha mara moja.

‘’kuna utaratibu na siyo kama nazuia maji yasitume lakini kuna bodi ya maji ya mto rufiji inafanya kazi vizuri na kuna taratibu zake ukitaka kumwagilia maji nenda ofisi zao na unapewa utaratibu na unakuwa mtanzania mzalendo.

"wewe unayelima na kumwagia mazao yako ufanikiwe basi usiwe kikwazo kwa watumiaji wengine wa maji majumbani kwa sababu ukitaka kuyavuta yote shambani kesho yake mradi, majengo makubwa na usambazaji mabomba yenye thamani ya mabilionji ya fedha itakwama, wewe unachepusha maji kwenye chanzo yatafikaje kwenye matenk na kusistiza tuache kuchepusha maji, alisema Meryprisca.

Aidha, alionya wananchi wanaolima ‘vinyungu’ kwenye vyanzo vya maji kuacha tabia hiyo na kueleza kuwa, mtu yeyote anayelima maeneo ya vyanzo maji ni adui namba moja wa zile jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu anasababisha maji kukauka na kusababisha miundo mbinu inayotolewa kwa ajili ya miradi ya maji kukosa thamani.

Kwa mujibu wa Meryprisca, shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ni mwiko na haviruhusiwi kwa kuwa zinasababisha maji kukauka huku lengo la serikali kupitia wizara yake likiwa kuendelea kupata maji zafi na salama.

Pia Naibu wa Waziri wa Maji aliwataka wananchi kulinda na kutunza wanatunza vyanzo vya maji na kuacha kabisa kufanya shughuli zozote za kibinadanamu kwa kuwa zinaweza kuharibu vyanzo hivyo alivyovieleza vinahitaji uoto wa asili ili viweze kuimarika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post