SIMBA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS*********************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imeffanikiwa kuichapa Tanzania Prison kwa bao la dakika za lala salama kupitia kwa kiungo wake Jonas Mkude akipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Kibu Denis dakika ya 86 ya mchezo.

Mchezo huo ambao ulichezawa katika dimba la Sokoine Mbeya, Tanzania Prison walikuwa wenyeji waliweza kuwazuia Simba kutopata bao kwa dakika zote kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili licha ya jitihada za kuzuia waliweza kufungwa bao moja.

Simba Sc imejikusanyia pointi 10 sawa na Yanga ambao hapo jana waliweza kushinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post