HKMU, WKU WAANZISHA USHIRIKIANO

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Profesa Yohana Mashalla, akimpa zawadi mwenzake wa Chuo Kikuu cha Western Kentucky cha Marekani (WKU), Profesa William Mkanta, wakati ujumbe wa chuo hicho ulipotemebelea HKMU kwaajili ya kuanzisha ushirikiano. Wengine ni Profesa John Sunnygard na Profesa Tania Basta wa chuo cha WKU.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Prof. Yohana Mashalla, akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Western Kentucky Marekani, Prof William Mkanta wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni profesa John Sunnygard kutoka chuo hicho. Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Western Kentucky cha Marekani wakiwa kwenye picha ya pamoja na na viongozi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), walipotembelea chuo hicho kwajili ya kuanzisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali za masomo

Profesa John Sunnygard wa Chuo Kikuu cha Western Kentucky cha Marekani (WKU) akimpa zawadi Makamu Mkuu wa HKMU, Profesa Yohana Mashalla walipotembelea chuo hicho jana kwaajili ya kuanzisha ushirikiano wa kitaaluma, kulia ni Profesa William Mkanta wa na Profesa Tania Basta wa chuo cha WKU.

***********************

Na Mwandishi Wetu

CHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Western Kentucky cha Marekani (WKU) kwaajili ya kuendeleza ushirikiano katika taaluma baina ya vyuo hivyo.

Hayo yalisemwa jana chuoni hapo jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Yohana Mashalla, wakati ujumbe wa chuo hicho ulipotembelea HKMU Mikocheni Dar es Salaam.

Alisema kwenye ushirikiano huo watajikita kwenye ushirikiano wa tafiti mbalimbali kwenye masuala ya afya na kuandika mapendekezo ya kuomba fedha kuwezesha kufanya tafiti zinazohitajika nchini.

Alisema ushirikiano huo utaijengea uwezo mkubwa HKMU wa kuandia maandiko ambayo yanaweza kuwavutia wadau mbalimbali duniani kutoa fedha za kusaidia tafiti kwenye masuala mbalimbali.

Alisema katika ushirikiano huo wataweza kuchapisha matokeo ya tafiti hizo ambayo yatasiadia sana kueleza ambacho HKMU inafanya kwenye tafiti hivyo kusaidia chuo kuonekana ulimwenguni kwmaba kinawexa kufanya tafiti.

“Sisi HKMU tuna malengo matatu, kufundisha, kufanya tafiti na kutoa ushauri kwenye taasisi za serikali na mashirika ya nje kwa kutoa mawazo na uzoefu wetu kwenye nyanja mbalimbali hivyo ushirikiano huu utatujengea uwezo kutoa ushauri mzuri kwa serikali na wengine,” alisema

Alisema kwenye mazungumzo yao wamebadilishana uzoefu wa namna ya kufundisha na teknolojia za aina mbalimbali zinazotumika kufundishia wanafunzi wa udaktari, uuguzi na fani zinginezo.

Alisema mmoja wa wafanyakazi wa WKU ni mtanzania ambaye alisoma Tanzania na kumalizia masomo yake nchini Marekani na ndiye aliyekuwa nguzo ya kuanza kwa ushirikiano na HKMU.

“Uhusiano huu unamanufaa kwetu na kwao kwasababu kwa dunia ya sasa ni ngumu sana taasisi kuishi kama iko kwenye kisiwa hivyo lazima taasisi zishirikiane. Hapa tunasikilizana wao wana kozi gani nasisi tunakozi gani tushirikiane kuanzisha program ambazo wao wanazo sisi hatuna,” alisema

Alisema kupitia ushirikiano huo watakuwa na utaratibu wa kubadilishana wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho kwa wao kuja kufundisha kwa muda kwenye fani ambazo hazina wataalamu wengi nchini.

Profesa William Mkanta, ambaye ni mtanzania anayefanyakazi kwenye chuo hicho cha WKU, alisema aliamua kuwaunganisha ili waweze kushirikiana kwenye tafiti zenye manufaa kwa jamii.

“Mimi ni mzaliwa wa Tanzania ila nafanyakazi Marekani kama Profesa nimeona umuhimu wa vyuo vikuu kusaidia jamii kwasababu vyuo vikuu ndiyo kitovu cha utafiti, huduma na kitovu cha kujifunza,”

“Ndiyo maana tumeona tuwe na uhisino wa vyuo hivi ili tuweze kuhamisha vipaji vilivyopo kwenye vyuo hivi. Dunia ni kama kijiji siyo lazima watu majirani ndiyo mshirikiane bali hata walio mbali wanaweza kushirikiana ndiyo maana tumeona umbali uliopo baina ya HKMU na WKU siyo kikwazo cha ushirikiano,” alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post