AFARIKI KWA AJALI AKIMFUKUZIA MUME WAKE BAADA YA KUMUONA NA MCHEPUKO

Picha ya Mke aliyefariki akiwa na mume wake

Ajali iliyopelekea kifo cha Mwanamke huyo

MWANAMKE mmoja kutoka nchini Nigeria amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari wakati akimfukuzia mumewe aliyekuwa na mwanamke mwingine kwenye gari hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shuhuda wa tukio hilo, mwanamke huyo alimuona mume wake huyo akitoka kwenye saluni ya kike na mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ni mchepuko wa mwanaume huyo ambapo mara baada ya kuwaona, mwanamke huyo alikimbia na kuingia kwenye gari lake na kisha kuliondoa kwa kasi akiwa na lengo la kuwahi ili akasimame mbele yao na kuwazuia kupita, jambo ambalo halikufanikiwa na hivyo kujikuta akipata ajali mbaya.

Mara baada ya ajali hiyo kutokea, mwanaume huyo alisimamisha gari lake na kisha kumshusha mwanamke aliyekuwa naye na baada ya hapo ndipo alikwenda kumsaidia mke wake ambaye alikimbizwa hospitali baada ya kuokolewa, mwanamke huyo alipoteza maisha baadaye akiwa hospitalini akipatiwa matibabu zaidi kufuatia ajali aliyoipata.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post