SHIKUBA ACHAGULIWA MWENYEKITI WA WAZAZI SHINYANGA VIJIJINI

 Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JUMUIYA ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini imefanya uchaguzi wa kuchagua Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo pamoja na wajumbe wawakilishi kwenye nafasi mbalimbali.

Uchaguzi huo umefanyika leo Septemba 25, 2022 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi mkuu wa uchaguzi Benard Reuben Shigela, amemtangaza Hamis Shikuba kuwa ndiye Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

“Natangaza matokeo ya nafasi ya Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini, kura zilizopigwa ni 486 hakuna iliyoharibika Mgombea wa kwanza ni Perepetua Masesa amepata kura 61, na Hamis Shikuba amepata kura 425, hivyo mshindi ni Hamis Shikuba ambaye ndiye Mwenyekiti mpya wa Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini,” amesema Shigela.

Aidha amemtangaza bwana Awadhi Aboud kuwa ameshinda nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa Wazazi Taifa, na Kashinje Komanya ameshinda nafasi ya Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM wilaya, pamoja na Leticia Masalu ameshinda nafasi Mjumbe Mkutano Mkuu wazazi Mkoa.

Wengine waliotajwa kushinda ni wajumbe watatu wa Baraza la wazazi wilaya, kuwa ni Nyamizi Robert, Leonarld Waziri na Mathias Rugata, aliyeshinda Mjumbe Mkutano Mkuu CCM Mkoa ni Mrisho Hamadi Mrisho, pamoja na Mjumbe UVCCM ni Jilunguya Ngelya.

Mwenyekiti huyo mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Hamis Shikuba, akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa ameshinda kiti hicho, ameomba ushirikiano na mahusiano mazuri katika kazi ili kuisukuma Jumuiya hiyo kusonga mbele.
Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Benard Reuben Shigela akitangaza matokeo ya uchaguzi, kwenye uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Benard Reuben Shigela akitangaza matokeo ya uchaguzi, kwenye uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Wajumbe wakimpongeza mshindi wa nafasi ya Uenyekiti Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Awali wagombea wa nafasi ya Uenyekiti Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini wakijinadi kwa wajumbe hapa ni Bwana Hamisi Shikuba akimwaga sera zake kwa wajumbe.

Perepetua Masesa (kulia) akimwaga Sera zake kwa wajumbe.

Wajumbe wakipiga kura kuchagua wagombea.

Zoezi la upigaji kura likiendelea.

Zoezi la upigaji kura likiendelea.

Zoezi la upigaji kura likiendelea.

Zoezi la upigaji kura likiendelea.

Zoezi la upigaji kura likiendelea.

Zoezi la upigaji kura likiendelea.

wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi

wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post