DC MBONEKO AKAGUA MIRADI YA MAJI VIJIJI VYA MWANDUTU, MWASHAGI INAYOTEKELEZWA NA RUWASA..."ITUNZENI, MSIIHUJUMU"Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maji kijiji cha Mwandutu

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akifungua maji katika kijiji cha Mwashagi wilayani Shinyanga, mradi ambao umetekelezwa na RUWASA na kutoa huduma ya maji kwa wananchi, (kulia) ni Mwananchi Maguta Jilili, (katikati) ni Diwani wa Kata ya Lyabukande Luhende Kawiza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji Kata ya Solwa na Lyabukande wilayani Shinyanga, huku akiwataka wananchi waitunze miundombinu ya maji.

Amefanya ziara hiyo leo Septemba7,2022, kwa kukagua utekezaji wa Mradi wa Maji Safi na Salama, katika Kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa na Kijiji cha Mwashagi Kata ya Lyabukande Miradi ambayo inatekelezwa na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Shinyanga.

Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, Mboneko  amewataka waitunze miundombinu ya Miradi hiyo ya Maji, ili idumu kwa muda mrefu kuwahudumia na kuondokana na adha ya matumizi ya maji machafu.

"Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda sana wananchi wake, na ndiyo maana amekuwa akitafuta fedha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo hii ya maji, na anatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo," amesema Mboneko.

"Nawapongeza pia wananchi kwa kutoa maeneo yenu na kupitisha mabomba ya maji, huu ndiyo uzalendo tunaoutaka, na muitunze miundombinu hii ya maji na kutoihujumu, na atakayeiharibu tutamchukulia hatua kali", ameongeza.

Katika hatua nyingine Mboneko, amewataka wananchi wanapotaka kuunganisha maji majumbani mwao, wawatumie wataalamu na siyo kutumia vishoka.

Naye Meneja Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijiji (RUWASA) wilayani Shinyanga Mhandisi Emmael Nkopi, amesema mradi wa maji katika kijiji cha Mwandutu asilimia kubwa umekamilika na utaanza kutoa huduma ya maji ndani ya mwezi huu.

Amesema Mradi wa Maji katika kijiji cha Mwashagi, wenyewe umekamilika na kuanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo, wameipongeza Serikali kwa kutekeleza Miradi hiyo ya Maji na kuwaondolea adha ya kutumia maji machafu pamoja na kutopoteza tena muda mrefu wa kufanya shughuli za maendeleo kwa sababu ya kufuata maji vijiji vya jirani.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maji kijijini humo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wanawake wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maji kijijini humo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wanawake wa kijiji cha Mwashagi Kata ya Lyabukande wilayani Shinyanga, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Maji kijijini humo.

Diwani wa Solwa Awadhi Mbaruku akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa Miradi ya Maji.

Diwani wa Lyabukande Luhende Kawiza akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa Miradi ya Maji.

Meneja Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Shinyanga Emmael Nkopi akielezea utekelezaji wa miradi ya maji kwenye ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (katikati) akiwa katika kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Mwandutu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa katika Tenki la Maji katika kijiji cha Mwashagi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akiendelea kukagua mabomba katika Tenki la Maji katika kijiji cha Mwashagi, (kushoto) ni Meneja wa RUWASA Emmael Nkopi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akiendelea kukagua mabomba katika Tenki la Maji katika kijiji cha Mwashagi, (kushoto) ni Meneja wa RUWASA Emmael Nkopi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akiendelea kukagua mabomba katika Tenki la Maji katika kijiji cha Mwashagi, (kushoto) ni Meneja wa RUWASA Emmael Nkopi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akifungua maji katika kijiji cha Mwashagi, (kulia) ni Diwani wa Lyabukande Luhende Kawiza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akimtwisha ndoo ya Maji Mwanamke Mbara Minza mkazi wa kijiji cha Mwashagi mara baada ya kukagua mradi wa maji kijiji humo ambao umeanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akimbebesha dumu la maji Mwananchi Shitula Ngassa Mkazi wa kijiji cha Mwashagi, mara baada ya kukagua mradi wa maji kijiji humo ambao umeanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akimbebesha ndoo ya maji Mwananchi Maguta Jilili Mkazi wa kijiji cha Mwashagi, mara baada ya kukagua mradi wa maji kijiji humo ambao umeanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Wanawake wa kijiji cha Mwashagi Kata ya Lywabukande wilayani Shinyanga wakiwa wamebeba ndoo ya maji.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja mara baada ya kukagua mradi wa maji na Tenki katika kijiji cha Mwashagi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja mara baada ya kukagua mradi wa maji na Tenki katika kijiji cha Mwashagi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post