SIMBA SC YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA KMC, YATOKA SARE 2-2


********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya KMC ambapo mchezo huo ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba Sc ilianza kupata bao la mapema kabisa kupitia kwa mshambuliaji wake Moses Phiri katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Kipidi cha kwanza kilimalizika huku Simba Sc ikiwa mbele ya bao 1-0 ikawapa matumaini ya kushinda mechi hiyo. Kipindi cha pili kilianza KMC wakionekana kabisa kuhitaji kusawazisha bao kwa kulisakama lango la Simba na baadae wakabahatika kusawazisha bao na dakika chache baadae wakapata bao la pili na kuongoza 2-1.

Simba Sc ilifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa ambapo miongoni mwa wachezaji walioingizwa ni Kyombo ambaye mabadiliko yake yalizaa matunda kwani ndiye aliyeweza kusawazisha bao na ubao kusomeka 2-2

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post