YANGA SC YAICHAPA COASTAL UNION, MAYELE AENDELEA KUTOA DOZI


*****************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imeendelea kutoa dozi kwenye ligi ya NBC mara baada ya hii leo kuichapa timu ya Coastal Union kwa mabao 2-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha.
Ni Mayele tena ambaye aliingia kipindi cha pili na kupachika bao la pili kwenye mchezo huo akipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Mkongo beki kisiki mwenzake Shaban Djuma na kuzamisha moja kwa moja nyavuni.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Benard Morrison kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka Jesus Moloko ambaye pia aliumia kwenye mchezo huo na kulazimishwa kutoka baada ya kuchezew rafu mbaya na mlinzi wa Coasta Union

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments