KARANI WA SENSA HAJAFIKA KWAKO?? ZIMEONGEZWA SIKU 7 ZAIDI. . FANYA HIVI KUPITIA SIMU YAKO

 Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 29,2022 wakati akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa zoezi ambalo lilitakiwa kuisha leo. Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 29,2022 wakati akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa zoezi ambalo lilitakiwa kuisha leo.
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema asilimia 93.45 ya kaya zote Tanzania zimehesabiwa hadi kufikia leo Jumatatu Agosti 29, 2022 saa 2 asubuhi na hivyo wameamua kuongeza muda wa ziada wa siku 7 kukamilisha zoezi hilo.


“Zoezi la kuhesabu watu lililoanza usiku wa kuamkia tarehe 23 Agosti 2022 hadi kufikia 29 Agosti, 2022 linaendelea vizuri ambapo kiwango cha kaya ambazo zimehesabiwa kimefikia asilimia 93.45. Haya ni mafanikio makubwa yaliyotokana na utayari mkubwa wa wananchi kushiriki kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi” amesema Makinda.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa taarifa hiyo Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda amesema zoezi la kuhesabu watu linatarajiwa kukamilika hii leo lakini kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa wafike katika ofisi za serikali ya mtaa au kupiga simu namba 0753-665491au 0626-141515 ,0784665404,0656279424 kutoa taarifa zao kwa karani wa sensa na atawafikia kuwahesabu na zoezi hilo litadumu kwa siku saba kuanzia Agosti 30-5


Ameongeza kuwa ifikapo Agosti 30-1 Septemba kutakuwa na zoezi la sensa ya majengo yote ikiwa ni pamoja na ofisi ili kuipa nafasi serikali kuboresha sera yake ya makazi hivyo ametumia fursa hiyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi.


"Wananchi ambao hajahesabiwa hakikisheni licha ya kuachiwa fomu za kujaza mtumie fursa hii kwa kupiga simu kwani waratubu na makarani wote wako kazini muhesabiwe ni kwa faida yenu na nchi kiujumla nafasi bado ipo",amesema.


Naye, mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu katika Ofisi za Taifa ya Takwimu Bi. Emilian Karugendo amesema makarani wa vijijini ndiyo waliopewa power bank kwa ajili ya Vishikwambi vyao kutokana na changamoto ya baadhi ya maeneo yao bado umeme haujafikiwa wanaofanya maeneo ya mijini wao umeme upo kila mahali na tumekuwa tukiwapigia Tanesco kama kuna hitilafu ya umeme.


Aidha vinavyotumika katika shughuli ya sensa baada ya kazi hiyo vitatumika kwa mpango Maalumu wa kiserikali huku akiwatoa hofu Makarani wote watalipwa malipo yao baada ya kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

2/Post a Comment/Comments

  1. Kwa nini makarani wa sensa wasilipwe stahiki zao wakati wakiendelea na kazi? Kwa nini iwe ni baada ya zoezi??

    ReplyDelete
    Replies
    1. wanaheshimu mikataba yao..sababu mikataba ilisema wazi kua watalipwa baada ya kazi

      Delete

Post a Comment