WAHUNI WAVAMIA MAKARANI WA SENSA NA KUWAPORA VISHIKWAMBI


Wakati sensa ya Watu na Makazi ikiendelea nchini, makarani wawili wamejikuta katika wakati mgumu baada kuporwa vifaa vyao vya kukusanyia taarifa maarufu kama vishikwambi na vibaka.


Tukio la kwanza limetokea jijini Arusha ambapo karani aliyetambuliwa kwa jina la Saraphia Kiwango ameporwa kishikwambi chake alipokuwa akielekea kuanza kuhesabu makundi maalum katika Kata ya Unga Ltd jijini Arusha huku mumewe akijeruhiwa kichwani na vibaka waliokuwa kwenye bodaboda.


Katika halmashauri ya Mpimbwe kata ya Majimoto mkoani Katavi, karani aliyetajwa kwa jina la Kenani Kasekwa amevamiwa na mtu asiyejulikana na kumwibia kishikwambi na fedha taslimu Sh760,000.

Inaelezwa kuwa alivamiwa baada ya kitasa cha mlango wake kuvunjwa na mwizi huyo kupora vitu hivyo huku ikidaiwa kuwa 
 inavyoonekana mwizi huyo alipuliza dawa ili walale usingizi fofo akapata mwanya wa kuiba pia redio aina ya subwoofer na simu.

CHANZO - MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post