ASKARI POLISI ALIYEPIGA MTUHUMIWA WA WIZI WA SIMU AKAMATWA

TAZAMA VIDEO HAPA 


Jeshi la Polisi limelaani kitendo kilichofanywa na Askari Polisi baada ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana mmoja akipigwa na askari huyo, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.Taarifa hiyo liyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David A. Misime, Makao makuu ya Polisi Dodoma, imeeleza kuwa kijana anayeonekana kwenye video hiyo akipigwa, alituhumiwa kuiba simu ambayo alikiri kuiba na kwenda kumuonyesha mtu aliyemuuzia ambaye pia alikutwa na simu hiyo.


Aidha, Jeshi limesema askari huyo aliyehusika na kitendo hicho tayari yuko mahabusu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.Jeshi limesisitiza kuendelea kusimamia nidhamu, haki, weledi na uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari polisi anayekiuka sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post