MWENGE WA UHURU WAMULIKA MRADI WA MAJI NYAMILANGANO UNAOTEKELEZWA NA RUWASA KAHAMA


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata Utepe kwenye Mradi wa Majisafi na salama wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao unatekelezwa na RUWASA.

Na Marco Maduhu, USHETU

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, ameweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Majisafi na salama Katika kijji cha Ididi Kata ya Nyamilangano Ushetu wilayani Kahama ambao utaondoa adha ya ukosefu wa maji kwa wananchi.



Mradi huo wa Maji umewekewa Jiwe hilo la Msingi Julai 31,2022 na Mwenge wa Uhuru, huku wananchi wakionyesha furaha ya kupata mradi huo wa Majisafi na salama, ambao unatekelezwa na Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wenye thamani ya Sh.milioni 350.

Akizugumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la Msingi Kiongozi huyo wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amesema mradi huo wa Maji una manufaa makubwa kwa wananchi, kuwaondolea adha ya ukosefu wa Maji na kuagiza ukamilishwe kwa wakati.

"Mradi huu wa maji ni mzuri tumeukagua ila naagiza ukamilishwe kwa wakati, ili wananchi wapate huduma ya Maji haraka na kutekeleza dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo kichwani Mwanamke," amesema Geraruma.

Naye Meneja Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira RUWASA wilayani Kahama Magili Maduhu, amesema mradi huo wa Maji ni wa Kisima kirefu na utekelezaji wake kwa sasa ni asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu na utanufaisha wananchi 5,296.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, amesema mradi huo wa maji ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa wananchi wa Nyamilangano na vijiji jirani na kuwataka wananchi wautunze mradi huo.

Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika mwaka wa fedha (2022-2023) ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kukamilisha miradi yote ya Maji ambayo ipo Halmashauri ya Ushetu.

Nao baadhi ya wananchi wa Nyamilangano akiwamo Sophia Boniphace ,wameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo wa Majisafi na salama ambao umewaondolea changamoto pia ya Mgogoro ya kifamilia sababu ya kufuata Maji umbali mrefu.

Aidha, Mwenge huo wa Uhuru leo umekabidhiwa mkoani Tabora.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao umetekelezwa na RUWASA.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye mradi huo wa Maji.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye mradi huo wa Maji.
Meneja wa RUWASA wilayani Kahama Mhandisi Magili Maduhu, akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo wa Maji.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akitetea jambo na mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao unatekelezwa na RUWASA.
Tenki la kuhifadhia Maji kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmshauri ya Ushetu.

Mwenge wa Uhuru ukiwa kwenye Mradi wa Maji wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments