MWENGE WAPITIA MIRADI KABAMBE HALMASHAURI YA USHETU

 


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Ushetu.

Na Marco Maduhu, USHETU

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye Miradi ya maendeleo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Mwenge huo wa Uhuru umekimbizwa jana Julai 31, 2022 katika Halmashauri ya Ushetu umbali wa Kilomita 70 na kupitia Miradi ya maendeleo Mitano yenye thamani ya Sh. bilioni 1.2.

Akizungumza wakati uzinduaji na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi hiyo ya maendeleo, Geraruma  amepongeza utekelezaji wake, na kubainisha kuwa ile ambayo ameitolea maagizo ukamilishwe haraka na kutoa huduma bora kuwa wananchi.

"Kuna baadhi ya Miradi ambayo nimeitolea maagizo ya kufanyiwa marekebisho naomba utekelezaji wake ufanyike haraka sana," amesema Geraruma.

Katika hatua nyingine Geraruma, amewasisitiza Wananchi wa Ushetu, kuwa siku ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi Agost 23 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa na kutimiza Malengo ya Serikali kupata idadi ya watu kamili.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, Lino Pius Mwageni, amesema Mwenge huo wa Uhuru ,utazindua ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Dakama.

Ametaja Miradi mingine ambayo umewekewa Jiwe la Msingi, kuwa ni ujenzi wa Barabara ya Nyamilangano kwa kiwango cha Lami Kilomita Moja, Utanuzi wa Mradi wa Majisafi na salama.

Miradi mingine ni uwekaji Msingi ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Ushetu, pamoja na kiwanda kidogo cha kuchakata nafaka kilichopo Uyogo.

Aidha, Mwenge huo wa Uhuru ukiwa mkoani Shinyanga kuanzia Julai 26 mwaka huu, umepitia Jumla ya Miradi ya Maendeleo 38 yenye thamani ya Sh. bilioni 43.1 ambapo leo umekabidhiwa Mkoani Tabora.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza wakati wa kupitia Miradi ya Maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akizungumza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Ushetu.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Ushetu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akizundua Mradi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Dakama.

Vyumba vya Madarasa katika Shule ya Dakama Halmashauri ya Ushetu.

Ukaguzi ukiendelea katika vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Dakama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu ambao unatekelezwa na RUWASA.

Tenk la Mradi wa Majisafi na usafi wa Mazingira wa Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Ushetu.

Jengo la Wagonjwa wa dhahura katika Hospitali ya Ushetu.

Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Emmanuel Chacha, akishiriki utengenezaji wa Mlango katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura Halmashauri ya Ushetu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akikagua ujenzi wa Kilomita Moja ya Barabara ya Lami Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu.

Ukaguzi wa Barabara Kiwango cha Lami Nyamilangano ukiendelea, kabla ya kuwekewa Jiwe la Msingi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post