MAKAMBA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI TPDC ....AIPONGEZA KWA UMAHIRI

Picha wajumbe wa bodi ya TPDC wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa nishati January Makamba leo mara baada ya kuzindua bodi hiyo.

Na Woinde Shizza,Arusha


Waziri wa Nishati January Makamba amesema uendeshaji umahiri na umadhubuti wa uongozi wa shirika la TPDC, ni jambo ambalo serikali unalipa uzito wa hali ya juu.


Makamba ameyasema hayo wakati akizindua bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo jijini Arusha na kueleza kwamba uteuzi wa bodi hiyo unaakisi dira na malengo mapya ya serikali kwa shirika hilo kuelekea katika mafuta na gesi.


Amesema bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wake balozi Ombeni Sefue inakidhi nafasi ya TPDC katika maendeleo ya nchi, Dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.


"Dhamira yetu ni kuona shirika hili linatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu bali uendeshaji wa rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi" ,alisema Makamba.


Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni katibu mkuu Kiongozi mstaafu amesema wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda inavyotakiwa na sekta hii ili taifa liweze kunufaika na rasilimali zake za mafuta na Gesi tulizopewa na Mungu.


Mikakati iliyopo kwa sasa ni ile ya serikali na haijaanza leo tutaipitia kama bodi mpya tumefanikiwa wapi na changamoto ni zipi na zitatatuliwaje ili kazi iendelee vizuri kujenga TPDC yenye kusaidia serikali.


Awali Mkurugenzi wa Shirika la mafuta na Gesi nchi muhandisi James Maragio amesema kuwa miradi ya mafuta na Gesi itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi.


Alisema kuwa wana miradi mikubwa ikiwemo mradi wa bilion 40 ikiwemo mradi wa kujenga bomba la mafuta kutoka hoima Uganda ambao umeonyesha mafanikio pia kuna maradi wa kutafuta mafuta katika bonde la ufa ambao upo kwenye Mchakato.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments