KANISA KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA LAPATA MAPADRE WAPYA


MASHEMASI Watano ambao wanatarajiwa kupewa daraja la Upadre hapo kesho, na askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, leo wamekiri imani Katoliki mbele ya askofu na Kanisa,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utolewaji wa daraja la Upadre.

Mashemasi hao ambao ni Emmanuel Kimambo wa Parokia teule ya Shishiyu, Emmanuel Gembuya wa Parokia ya Buhangija, Paul Mahona wa Parokia ya Wila, Simon Lutamula wa Parokia ya Mwamapalala na Eliasi Vumba wa Shirika la Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisco (Wakapuchini) wamekiri imani na kutia saini viapo vyao kupitia ibada ya masifu ya jioni, ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma,Ngokolo mjini Shinyanga.
SAUTI ZA MASHEMASI WAKIKIRI IMANI


Akitoa mafundisho yake katika ibada hiyo, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,anewaomba waamini kuendelea kuwaombea Mashemasi hao ili watakapopewa daraja la Upadre ,waweze kutekeleza kwa uaminifu utume watakaokabidhiwa na kanisa.

Askofu Sangu amefafanua kuwa, daraja la Upadre ambalo watapewa hapo kesho, ni njia itakayowashirikisha katika huduma ya kikuhani ya kuokoa roho za watu na kuwatafuta wale waliopotea.
SAUTI YA ASKOFU SANGUMashemasi wakitia saini viapo vyao mbele ya AskofuMashemasi wakirudi katika nafasi zao baada ya kusaini viapo vyaoVicar wa Shirika la Wakapuchini kanda ya Tanzania Pd.Paschal Vincent Dohho (mwenye kanzu ya Ugoro) akiwa katika ibada ya masifu ya jioni Kanisa kuu NgokoloAskofu Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Mashemasi mara baada ya Ibada ya Masifu ya jioni(Kushoto ni Katibu wa askofu Pd. Deusdedith Kisumo na Kulia ni Paroko wa Parokia ya Mwadui Pd.Michael Msabila)

Chanzo - http://radiofaraja.com/

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post