WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA DIT

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba (mwenye koti) akimuelezea jambo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa anakagua bidhaa za vipuri zinazotengenezwa DIT kwaajili ya kutumika kwenye pikipiki na bajaji akiwa kwenye ziara yake kutembelea Taasisi hiyo leo julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam.

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Julai 28,2022 amefanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kujionea ukuzaji wa teknolojia kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo mara nyingi hutengenezwa nje ya nchi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha kujifunzia DIT, Waziri Mkenda amesema kuwa teknolojia ambazo wamekuwa wakiibuni DIT wanatakiwa waangalie uwezekano kuibiasharisha na baadae kuiingiza sokoni.

Amesema amejionea ni namna ggani DIT wanatengeneza vipuri ambavyo vinatumiwa hasa kwenye bajaji na pikipiki na hata kwa baadhi ya magari na kufungua milango ya kufanya uhamisho wa teknolojia kutoka nje kwa kujifunza hapa nchini na kuibiasharisha.

Vipuri hivyo wanatengeneza kwa kutumia chupa za plastiki ambazo zimetupwa na kuzichukua kuziyeyusha na kutengeneza piletes ambazo zinasaidia kutengeneza vipuri hivyo ambavyo hutumika kwenye pikipiki,bajaji na hata kwenye magari.

Amepongeza uongozi wa Chuo hicho kuendelea kuibua bunifu mbalimbali ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa vijana na taifa kwa ujumla kwani kunaweza kusaidia kuokoa fedha nyingi za kigeni.

"Tukiendelea hivi, baadae tunaweza kusema tuzalishe pikipiki zetu, tusikimbilie kusema tunazalisha pikipiki, wenzetu India na China walianza hivihivi kabla ya kuanza kutengeneza pikipiki na magari. Leo mnatengeneza vipuri baadae tutaweza kutengeneza pikipiki zetu". Amesema Waziri Mkenda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, (DIT) Mhandisi Dkt.Richard Masika amesema Taasisi ya Teknolojia kwa muda mrefu imekuwa ikitoa elimu nadharia zaidi baada ya hapo ikaweka msisitizo mkubwa kwa vitendo lakini wameona kwamba pamoja na kufanya hivyo bado wahitimu wamekuwa wanaajirika lakini hawawezi kujiajiri, kwahiyo wameona waende kwenye hatua nyingi kwa kuwafunza wanafunzi kwa kuwatengenezea mazingira ya kiwanda na kufanya kazi za uzalishaji kwenye kiwanda hatua kwa hatua na zile bidhaa zinazotoka zinakwenda kutumika.

Pamoja na hayo amesema kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za aina saba tofauti, uzaloishaji wake unategemeana zaidi na oda wanazokuwa nazo, bidhaa zinazozalishwa huchukuliwa hapo hapo na kwasasa watumiaji wengi wameshawafahamu na wanakwenda moja kwa moja hapo chuoni kuchukua bidhaa hizo

Amesema wanachokifanya sasa ni kuyaweka vizuri mazingira ya uzalishaji ili kiwanda hicho kiwe halisi cha uzalishaji hivyo kumsaidia mwanafunzi anapotoka hapo anakuwa tayari kuingia kiwandani bila hofu yoyote

"Kwa mwaka huu tumepanga kuzindua viwanda viwili, kiwanda kimoja ni hiki ambacho tunakifanyia majaribio na kiwanda cha pili kitakuwa Mwanza ambacho kitakuwa kinazalisha bidhaa za ngozi na itaanzia kwenye hatua ya chini kwa maana ya kuitibu ile ngozi na kuikausha na baadae kutengeneza bidhaa nyingi zaidi". Amesema Mhandisi Dkt.Masika.

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba (mwenye koti) akimuelezea jambo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa anakagua bidhaa za vipuri zinazotengenezwa DIT kwaajili ya kutumika kwenye pikipiki na bajaji akiwa kwenye ziara yake kutembelea Taasisi hiyo leo julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba (mwenye koti) akimuelezea jambo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa anakagua bidhaa za vipuri zinazotengenezwa DIT kwaajili ya kutumika kwenye pikipiki na bajaji akiwa kwenye ziara yake kutembelea Taasisi hiyo leo julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, (DIT) Mhandisi Dkt.Richard Masika (kulia) akionesha kitu katika mtambo wa kuzalisha vipuri vya kwenye pikipiki na bajaji mara baada ya Waziri kufanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba (mwenye koti) akimuelezea jambo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa anakagua bidhaa za vipuri zinazotengenezwa DIT kwaajili ya kutumika kwenye pikipiki na bajaji akiwa kwenye ziara yake kutembelea Taasisi hiyo leo julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, (DIT) Mhandisi Dkt.Richard Masika (kulia) wakati alipotembelea kiwanda cha kujifunzia uzalishaji wa bidhaa DIT leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akioneshwa baaddhi ya vipuri vinavyotengenezwa DIT kwaajili ya kutumika kwenye pikipiki na bajaji mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, (DIT) Mhandisi Dkt.Richard Masika akizungumza mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda mara baada ya Waziri kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) mara baada ya kufanya ziara kwenye Taasisi hiyo leo Julai 28,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post