RAIS DKT. MWINYI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MTANGAZAJI WA ZBCRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu jamaa wa marafiki kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa ZBC televisheni, Bi.Sharifa Maulid.


Katika salamu hizo za pole, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na kifo cha mtangazaji huyo mkongwe na kuisihi familia ya marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.


“Natoa mkono wa pole kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa ZBC televisheni, marehemu bibi Sharifa Maulid, naukumbuka umahiri wake katika utangazaji kwani alikuwa hodari katika kazi yake hiyo na kazi zake nyingine alizozifanya mbali ya utangazaji,”ilieleza sehemu ya salamu za pole alizozitoa Rais Dkt.Mwinyi.


Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewasihi watangazaji na wafanyakazi wote wa sekta ya habari nchini kufuata nyayo na uzalendo wa marehemu bibi Sharifa Maulid ambaye hadi anafariki dunia alikuwa Afisa Habari katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.


Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post