WANANCHI TABORA WAANZA KUNUFAIKA NA HUDUMA MPYA YA NI - KONEKT KUPATA HUDUMA ZA UMEME


Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora Mhandisi Hadija Mabrouk
    
Meneja Masoko TANESCO Mwl. Mussa Kassim

Wakazi wa Mkoa wa Tabora wamefurahishwa na hatua ya kuanza kufaidika na huduma mpya ya kupata huduma za kwa njia ya kidigitali ya shirika la umeme nchini TANESCO  ambayo imeanza  kutumika hivi karibuni inayojulikana kama Ni- konekt. 

Meneja  masoko wa shirika hilo  kutoka Makao makuu Dodoma  Mwl. Mussa Kassim akiwa mkoani Tabora  alielezea huduma hiyo kuwa ni rahisi  na inapatikana  kupitia kompyuta  na simu za kiganjani ambapo mwananchi anaweza kuomba   na kunganishiwa huduma ya umeme bila kufika katika  ofisi za shirika .


Pia amesema huduma hiyo ni msaada mkubwa kwa wananchi ambao wakati mwingine wamekuwa wakikutana na matapeli katika mazingira ya kutafuta huduma ya kuunganishiwa umeme.


Mmoja  kati ya wanufaika wa huduma hiyo  mkoani Tabora Lucas  Shilima wakati  alipotembelewa  nyumbani kwake alisema  alitumia  huduma ya Ni- konekt na kuunganishiwa umeme nyumbani kwake ndani ya muda wa siku mbili.


Katika  hatua nyingine  meneja wa TANESCO  mkoa wa Tabora mhandisi Hadija  Mabrouck  amesema shirika linaendelea kuboresha  na kujenga miundo mbinu mipya  ya  huduma ya umeme katika Mkoa wa Tabora  na hivyo huduma ya  umeme ni ya uhakika  huku akiomba wawekezaji  katika mkoa huo kutokuwa na wasisi kuhusu huduma ya umeme.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments