TANZANIA YAPONGEZWA MAPAMBANO YA CORONA

Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Ted Chaiban 

             Na. WAF - Dar es Salaam 

KATIBU Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Ted Chaiban ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kupambana na UVIKO-19. 

Pongezi hizo amezitoa leo Julai, 5, 2022 nchini Tanzania baada ya kutembelea katika vituo vya kutoa chanjo ya UVIKO-19  ikiwemo zahanati ya Makangarawe na sehemu maalumu iliyotengwa kwaajili ya utoaji wa huduma ya chanjo katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

"Tanzania ilikua nyuma katika utoaji wa chanjo lkn sasa hivi kuna  muamko mkubwa umeongezeka kutoka asilimia 6.3 hadi kufikia asilimia 12.4 ya utoaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 niwapongeze sana." amesema Chaiban

Pia, ametoa pongezi kwa wauguzi na wahudumu kwa kuendelea kutoa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 pamoja na utoaji wa elimu katika maeneo hayo aliyotembelea na kuwasihi kuendelea kutoa huduma hiyo kwa kuwa ni kujali Afya za watanzania.

"UVIKO-19 ni ugonjwa hatari na bado unaendelea kuenea katika maeneo mbalimbali Duniani hivyo tuendelee kuchukua tahadhari na kutoa huduma ya chanjo hii." amesisitiza 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke (DMO) Dr. Irene Haule amesema wilaya yake imefanikiwa kuvuka kiwango cha utoaji wa huduma ya chanjo elekezi kutoka 3,500 hadi sasa kufikia idadi wa wapata huduma 7,000 kwa siku.

"Tumefanikiwa kutoa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 kutokana na mikakati tuliyonayo ikiwemo ya utoaji elimu kwa jamii, tumeweka mabanda matano ndani ya viwanja vya sabasaba, kutoa huduma nyumba kwa nyumba pamoja na kwenye vituo, wanapata huduma nyingine lakini na chanjo ya UVIKO-19." amesema Dkt. Haule

Aidha, Mikakati ya utoaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 ikiwemo utoaji wa elimu inasaidia kuongeza idadi ya watanzania kupata huduma hii ili kuendeleza jitihada za Serikali za kuwalinda wananchi na Magonjwa mbalimbali. 

Katibu Mkuu msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Bw. Ted Chaiban yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazo ya siku nne na ataendelea kutembelea maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam na Dodoma kwa lengo la kuhamasisha utoaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments