AMUUA MKE WAKIWA GESTI MGOGORO WA MICHEPUKOMWALIMU wa Shule ya Sekondari Tanga, iliyopo mkoani Tanga, Emmanuel Jerome (32), anadaiwa kumnyonga mke wake, Lucy Nshoma (34, katika nyumba ya kulala wageni mkoani Rukwa, kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kamba juu ya mti siku moja baadaye mkoani Katavi.


Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema marehemu ni mkazi wa Tanga na chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.


Kamanda Makame amesema marehemu Jerome alikuwa na mgogoro na mke wake, ambapo alimtuhumu kutoka kimapenzi na wanaume wengine.


Alisema Jerome na mkewe walipanga safari kuelekea mkoani Rukwa, ambapo ni nyumbani kwao marehemu mke wake na walifikia nyumba ya kulala wageni Julai 26, 2022, ndipo usiku alipochukua uamuzi wa kumnyonga mkewe.


Kamanda Makame alisema baada ya kumnyonga katika nyumba hiyo ya wageni, aliacha ujumbe wa maandishi kwa ndugu wa mke wake ambao ni mashemeji zake uliosomeka: "Nisameheni kwa yaliotokea".


Alieleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo mkoani Rukwa alikimbilia mkoani Katavi na Julai 27,2022, huko mtaa wa Ilembo, Manispaa ya Mpanda, alichukua uamuzi wa kujinyonga na walikuta mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post