BENKI YA NBC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA KADI YA MALIPO YA DOLA


Meneja wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NBC,Esnat Hollela akipeana mkono na Abel Kaseko, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mauzo wa NBC wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya malipo ya Dola inayowezesha malipo mtandaoni bila makato ya ziada.Kushoto ni Meneja wa Bidhaa na Mauzo wa NBC, Dorothea Mabonya na Ulrik Peter, Kaimu Mkuu wa Huduma za Kidigitali. Kadi hiyo ya USD Visa Debit Card itasaidia ufanyaji wa malipo ya huduma na bidhaa bila malipo ya ziada


Dar es Salaam, Julai 28, 2022.

Benki ya NBC leo imezindua kadi inayowezesha malipo mtandaoni kwa njia ya Dola.Kupitia kadi hii wateja wanapata fursa ya kufanya malipo ya bidhaa na huduma kwa dola pasipo makato ya ziada.


Ni mapinduzi ya tehama yanayowezesha malipo ya visa kadi inayohakikishia wateja usalama na urahisi pindi wafanyapo malipo ya mtandao.


Mkurugenzi msaidizi wa benki ya NBC,Elibariki Masuke,amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha wateja wao wanazifikia fedha zao kiusalama na wanakuwa na uwezo wa kufanya miamala kwa urahisi,kuboresha huduma zao.


”Kadi hii ni haraka, rahisi kutumia na salama,njia bora kabisa ya kufanya malipo na miamala ya kimtandao.Kadi hii inaondoa kero ya kubena fedha nyingi kwani hali hiyo huhatarisha usalama wa fedha hizo”.


“Tunayofuraha,kuzindua kadi hii ya malipo ya visa ya fedha za kimarekani,ambapo itaongeza ufanisi kwa wateja wetu na kuwezesha urahisi wa kufanya malipo na miamala ya dola za kimarekani,”Aliongeza.


Kwa kuzingatia matumizi na usalama,Masuke alisema kuwa kadi hii ya malipo ya visa ya dola za kimarekani ni rahisi na salama kwa kuwa zinalindwa na teknolojia ya 3D chip na pini za kisasa.


Mbali na kumwezesha mtumiaji wa kadi hiyo kufanya malipo ya mtandaoni bila malipo ya ziada,kadi hii pia ina uwezo wa kutumika kwenye makampuni ya Visa zaidi ya 2000(ATM)kwa Tanzania,zaidi ya kampuni milioni 2.7 za Visa Duniani kote na pia zaidi wafanyabiashara 24,000 wanaopokea malipo ya Visa kwa Tanzania. Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kadi za Benki ya NBC,Esnat Hollela alisema kuwa kadi hii inatumia malipo ya fedha za dola za kimarekani pia ina uwezo wa kulipia huduma kwa fedha nyingine. “Kwa malipo ya mtandao na tovuti,kadi hii inauwezo wa kufanya malipo yote ya kimtandao kama vile,Amazon,AliExpress,Alibaba, na kununua vifurushi kama vile Netflix,DSTV,na malipo mengine ya mtandao”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post