RAIS SAMIA AITAKA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KUFANYA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA ELIMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022. Taasisi hiyo iliyozinduliwa ina lengo la kumsaidia mtoto wa Kike Shuleni pamoja na Watoto wengine ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kielimu na kimaisha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein mara baada ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi na Wananchi baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi, Wanafunzi na Wananchi alipowasili katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022 kwa ajili ya kuzinduzia Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo yenye saini 50 za Wanafunzi Wanawake waliofaidika na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Wanu Hafidh Ameir akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kufanya mabadiliko katika mitaala ya elimu (syllabus).

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akizindua Taasisi ya Wanawake Initiatives Foundation (MIF) na kueleza kuwa Zanzibar inakabiliwa na changamoto nyingi katika sekta ya Elimu.

Aidha, Rais Samia ametaka pia kuwepo na umakini katika sifa za walimu wanaoajiriwa, utungaji wa mitihani pamoja na uwezeshwaji wa vitendea kazi kwa wakaguzi.

Rais Samia amesema licha ya ufaulu kupanda kiasi kwa mwaka 2021 na kupungua kwa idadi ya waliopata sifuri, bado iko haja kwa Wizara hiyo pamoja na wadau kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto zilizopo.

Rais Samia pia amewataka wazazi, walezi na jamii kubeba jukumu la kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo ipasavyo na kuhakikisha kuwa wanapata muda wa kujisomea.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameishukuru taasisi ya MIF kwa mchango na jitihada inazofanya katika kuinua kiwango cha elimu kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais Samia ametoa wito kwa Taasisi zingine zisizo za Serikali kuiga mfano wa MIF na kujitolea katika masuala ya kijamii hasa kwenye sekta ya elimu na malezi kwa watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments