SUA YAWAJENGEA UWEZO MAFUNDI SANIFU NCHINI KUHAKIKISHA UBORA WA BIDHAA ZA MIMEA DAWA

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji pamoja na Mkuu wa Mradi huo.
Mmoja wa wawezeshaji hao kutoka Denmark Prof. Christian Janfelt akielekeza jambo wakati akiwasilisha mada yake.
Mafunzo yakitolewa.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo huyo.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yakiendelea.


*************************


Na Calvin Gwabara, Morogoro


CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi sanifu zaidi ya 25 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali nchini kutumia vifaa vya kisasa vya kuongeza ubora wa bidhaa zitokanazo na mimea dawa ili ziweze kushika soko la ndani na nje na kuongeza pato la mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia mafunzo hayo Mkuu wa Mradi wa Mradi wa Matumizi ya Ubunifu ,uvumbuzi na teknolojia mbalimbali katika kuboresha bidhaa za mimea dawa ili kuboresha Maisha (GRILI) Dkt. Faith Philemon Mabiki kutoka SUA amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wataalmu hao kutoka zaidi ya taasisi saba nchini namna ya kutumia vifaa vya kisasa vya uchunguzi lakini pia kuweza kufanya marekebisho pale vifaa hivyo vinapoharibika.

“Ili bidhaa yoyote itoke kwenye soko la ndani iingie kwenye soko la kikanda na kimataifa swala la ubora ni muhimu sana na unapozungumzia ubora huwezi kukwepa matumizi ya vifaa vya uchunguzi na hawa tuliowakuleta hapa ndio wahusika wakuu wa kutumia vifaa hivyo kwenye taasisi zao nchini , hivyo tunahitaji wawe na uwezo wa kuvitumia lakini pia kuvifanyia matengenezo vinapoharibika” alisema Dkt. Mabiki.

Dkt. Mabiki ameongeza kuwa lengo linguine ni kutaka wafahamiane na kuweza kushirikiana wenyewe kwa wenyewe katika ya taasisi moja na taasisi nyingine katika kusaidiana pale mmoja anapopata changamoto katika kufanya kazi hizo na hata pale inapoharibika waweze kusaidiana.

Amesema kupitia yote hayo wnataka kuboresha ubora wa bidhaa za mimea dawa ili zishike soko na kuleta kipato kwa wat una taifa lakini pia kuwahakikishia watumiaji usalama na kufikia malengo ya taifa yam waka 2025.

Mradi wa GRILI umewezesha kununu na kufunga vifaa vya kisasa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo vyenye uwezo wa hali ya juu ya kupima ubora wa bidhaa zitokanazo na mimea dawa na bidhaa zingine ili kuhakikisha usalama wa bidhaa kwa watumiaji.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanaendeshwa na wawezashaji wane kutoka Chuo kikuu cha Copenhagen cha nchini Denmark ambao ni Prof. Christian Janfelt, Prof. Nickolaj Petersen,Prof. Bjarne Styrishave na Keneth Pedersen na yanafadhiliwa na Shirika la maendeleo la Denmark DANIDA kupitia Mradi wa GRILI katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments