Breaking : RAIS SAMIA AMTEUA JENERALI JACOB JOHN MKUNDA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments