GEORGE MPOLE AIBUKA MFUNGAJI BORA LIGI KUU YA NBC 2021/2022.... YANGA YATWAA UBINGWA BILA KUFUNGWA


George Mpole ameibuka Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2021/2022
Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Mtibwa Sugar

HATIMAYE Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC bila kupoteza mchezo wowote baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Mtibwa Sugar bao lililowekwa kimiani na Denis Nkane katika dakika ya 80.


Kwa matokeo hayo Yanga imemaliza msimu ikiwa na jumla ya alama 72 huku ikiwa na wastani wa magoli 40 ya kufunga na kufungwa.

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele akiwa katika harakati za kumtoka mlinzi wa Mtibwa Sugar

Baada ya mchezo huo Yanga itajiandaa kuelekea Jijini Arusha ambapo itakwenda kucheza dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


Kwa upande mwingine klabu ya Biashara United imeungana na Mbeya Kwanza kwa timu zilizoshuka daraja huku Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar zikinusurika kushuka na hivyo zitajiandaa kucheza Play-Off.

Aidha mshambuliaji wa Geita Gold FC George Mpole ameibuka mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu akiwa na jumla ya mabao 17 na pasi 4 za mabao huku akifuatiwa na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele aliyemaliza msimu akiwa na mabao 16 na pasi 5 za mabao.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments