TAASISI ZOTE ZINAZOTOA HUDUMA TIC KUTUMIA MFUMO WA DIRISHA MOJA KWA WAWEKEZAJI


Picha ya pamoja ya washiriki na wakuu wa taasisi zinazounda mfumo wa huduma za mahala pamoja (TIC) walipokutana Morogoro kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa Mradi wa Dirisha/Mfumo wa pamoja wa kuwahudumia wawekezaji.
Kamishina Jenerali wa uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala, akizungumza na waandishi wa habari Morogoro baada ya kikao cha pamoja cha wakuu wa Taasisi 12 zinazihusika na utoaji vibali mbalimbali kwa wawekezaji nchini
Dkt. Yusuph Ngenya Mkurugenzi Mkuu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akizungumza na waandishi wa habari Morogoro baada ya kikao cha pamoja cha wakuu wa Taasisi 12 zinazohusika na utoaji vibali mbalimbali kwa wawekezaji nchini
Mwakilishi wa kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. M. Bunini ameongoza kikao cha dharura cha wakuu wa taasisi zinazounda mfumo wa mahala pamoja (NIFC) kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa Mradi wa Dirisha/Mfumo wa pamoja wa kuwahudumia wawekezaji kilichofanyika Morogoro tarehe 07 June 2022.


"Serikali katika kuhakikisha inaboresha huduma ya uwekezaji hasa kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) imeandaa mfumo wa pamoja ambao utawezesha taasisi zinazotoa huduma kwa wawekezaji kusomana (Interface)", amesema Bw. Bunini.


Kikao hiki kimepitia taarifa za mfumo ulipofikia, kuwaonyesha wakuu wa taasisi mfumo unavyofanya kazi, kujadili usalama wa mfumo ikiwemo kupitia hati za makubaliano za kubadilishana taarifa ( Data sharing agreement).

Utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia tisini.

Meneja mradi wa mfumo wa kidijitali wa kuwahufumia wawekezaji Bw. Robert Mtendamema amesema "majadiliano ya leo yamelenga kukubaliana kuanza matumizi ya mfumo huo hivi karibuni".


Taasisi ambazo zitaanza kutumia mfumo huo kwa awamu ya kwanza ya mradi huo ni; BRELA, TRA, NIDA, UHAMIAJI, ARDHI, IDARA YA KAZI na kamishina wa kazi.


Dirisha/Mfumo huu utakapozinduliwa itasaidia, kutoa vibali kwa wakati, Itasaidia kuondoa urasimu, kutoa huduma za haraka kwa wawekezaji na utatunza taarifa za wawekezaji.


Kituo cha uwekezaji Tanzania kinafanya kazi pamoja na taasisi kumi na mbili za Serikali zinazotoa huduma mahala pamoja (NIFC ) taasisi hizo ni BRELA, NEMC, NIDA, TRA, UHAMIAJI, ARDHI, KAMISHINA WA KAZI, TANESCO, OSHA, TBS na TMDA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post