Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 14, 2022

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI YA ASFC...YAIFUATA KIBABE YANGA
Na Alex Sonna

SIMBA w wametinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) na kuifuata Yanga kibabe baada ya kuichapa mabao 4-0 Timu ya Pamba FC kutoka Mwanza Mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Peter Banda dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi ya Rally Bwalya bao lililopelekea Simba kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba ikinufaika zaidi na mabadiliko hayo.

Kibu Denis aliwanyanyua mashabiki wa Simba dakika ya 47 akifunga bao mara baada ya kupokea krosi ya Mohamed Hussein na mabaao mawili yamefungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 52 na 88.

Kwa ushindi huo Simba watakutana na Yanga Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Azam FC watakutana na Coastal Union.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages