SIMBA SC YAMPIGA CHINI MORRISON


KLABU ya soka ya Simba imeuarifu Umma hasa mashabiki wake na wapenzi wa soka nchini kuhusu hatima ya mchezaji wao Bernard Morrison

Klabu ya Simba Sc imetoa taarifa ya kumpa mapumziko mchezaji raia wa Ghana Benard Morisson hadi mwisho wa msimu taarifa hiyo imetolewa na Simba SC Mei 13, 2022.

Taarifa ya Simba imeeleza kuwa imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi.


Simba SC imetoa shukrani kwa Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu hiyo.

“Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klabu yetu na kuisadia kupata mafaniko kadhaa ikiwemo kucheza robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam Sports, na ubingwa wa kombe la Mapinduzi,” imeeleza taarifa ya Simba

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments