MPINZANI MKUU WA RAIS MUSEVENI WA UGANDA BOBI WINE AHUTUBIA BARAZA KUU LA CHADEMA TANZANIA.... ATAKA WAWEKEZE KWA VIJANA


Msanii na mwanasiasa wa Upinzani  nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ameutaka uongozi wa CHADEMA kuwekeza nguvu katika kukuza vijana huku akisema anaamini vijana ndio wanaojua kupambana kudai haki zao.

Akihutubia katika kikao cha baraza kuu la CHADEMA, Mlimani City jijini Dar es salaam kiongozi huyo amesema ipo haja ya vyama vya siasa hususani vya upinzani kuwekeza kwa vijana na kuwafundisha siasa za mageuzi.

Aidha kiongozi huyo amewataka CHADEMA na wananchi wa Uganda kuungana katika kuendesha siasa za mabadiliko na mageuzi.

"Tunahitaji kuweka vichwa vyetu pamoja sisi Uganda na watu wa Chadema tupambane kuleta mageuzi katika nchi zetu hizi mbili, nipo hapa kuwaambia watu wa Uganda wanaelewa mnayopitia na nawaambia tupo pamoja katika kupambana", amesema kiongozi huyo

"Kwa kuwa tumezielewa changamoto zetu zinazotukabili na tumezikubali, tumeamua kujenga umoja na muunganiko wa kupambana kwa pamoja kama ambavyo imefanyika huko nyuma, tuchague kuwa kizazi kipya cha kupigania uhuru ndani ya nchi zetu" amesisitiza mwanasiasa huyo mpinzani mkuu wa Rais Museveni nchini Uganda.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments