KESI YA WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA WA ETHIOPIA YAAHIRISHWA

Na Beatrice Mosses - Manyara

Hati 13 za mashitaka yanayowakabili wahamiaji haramu 13 raia kutoka nchini Ethiopia zimewasilishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara hii leo, ambapo kesi hiyo imehairishwa kutokana na changamoto ya ukosefu wa mkalimani wa lugha mbalimbali.

Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2022 inayowakabili wahamiaji hao kinyume cha sheria ya uhamiaji kifungu cha 45 kifungu kidogo cha kwanza (1) I kinachozuia kuingia nchini bila kuwa na kibali maalumu.

Wahamiaji hao walikamatwa April 27 mwaka huu huko wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara katika msako maalumu uliofanya na jeshi la polisi mkoani hapa.


Hata hivyo Wahamiaji hao haramu walifikishwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara kwa mara ya kwanza May 5 mwaka huu ambapo walisomewa mashtaka yanayowakabili ya kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kesi hiyo ipo chini ya Hakimu mkazi Martin Masao wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara pamoja na Mwendesha mashtaka wa uhamiaji mkoa wa Manyara Mkaguzi Yohana Malima, na kesi hiyo imehairishwa hadi May 16 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments