KAMUGUNDA : WAISLAM TUUENZI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA VITENDO

 

Alhaji Sheikh Hashim Kamgunda Mwenyekiti wa Taawanu Islamic Foundation  Tanzania, akizungumza na Waumini wa kiislam katika Msikiti wa Ijumaa Kata Katoro Halmashauri ya Wilaya Bukoba.

Alhaji Sheikh Hashim Kamgunda Mwenyekiti wa Taawanu Islamic Foundation  Tanzania, akizungumza na Waumini wa kiislam katika Msikiti wa Ijumaa Kata Katoro Halmashauri ya Wilaya Bukoba.
Wa kwanza kushoto ni Alhaj Bumalwa kutoka Wilayani Missenyi akiongoza waumini kusoma Mlango wa Maulidi, huku akitunzwa na Hajat Ziara baada ya kumkosha.
Baadhi ya waumini waliohudhuria
Mkurungezi wa Maji ya Kunywa ya Zahra, Hajjat Zahra ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taawanu Islamic Foundation International akizungumza
Baadhi ya wafanyakazi wa zahanati mpya ya Care & Cure wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Taawamu Islamic Faundation na Zahra Pure Drinking Water.

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Waumini wa Dini ya Kiislam wamekumbushwa kuendelea kuishi kwa kufanya Ibada na mambo ya Heri kama ilivyokuwa wakati wa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kufikia malengo ya Mwezi huo.


Akitoa nasaha zake katika Msikiti wa Ijumaa Kata Katoro Halmashauri ya Bukoba, Alhaji Sheikh Hashim Kamugunda Mwenyekiti wa Taawanu Islamic Foundation Tanzania, amewataka Waislam kuendelea kufanya mema kwani kumalizika kwa Ramadhan ni kipimo cha Uchamungu.


"Ndugu zangu Waislam Mwezi Mtukufu ulikuwa Darasa kwetu, tulikuwa Darasani tukijifunza, sasa baada ya masomo hayo tunatakiwa kufanya mtihani katika yale tuliyojifunza ili kufikia malengo ya funga (saumu) ambayo ni Uchamungu",amesema Alhaji Kamugunda.


Aidha Alhaj Kamugunda ambaye ni Mwenyekiti wa Taawanu Nchini Tanzania ambao ndio wamiliki wa Zahanati mpya inayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni, kuhusu Zahanati hiyo ya Care & Cure amesema kwamba, awali ilipangwa Uzinduzi wa zahanati hiyo ufanyike Mei 03, 2022 lakini wamesogeza mbele mpaka taratibu nyingine zikamilike.


"Tumekamilisha Taratibu zote za Vibali na Tumekwishalipia kila kitu, kinachosubiriwa ni Mamlaka kutoa Certificate (Cheti) ili tuweze kufungua Zahanati yetu itayohudumia Watu wa aina zote, bila kujali itikadi zao wala Dini zao na Zahanati hii itakuwa ikitoa huduma ya kupima magonjwa zaidi ya 17, mashine zote za kupimia zipo tayari na wahudumu (Daktari) wamekwishafika", amesema Kamugunda.


Baraza hilo limehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Masheikh na Wakufunzi pamoja na Mkurugenzi wa Taawanu International Hajat Zahra.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments