Breaking

Post Top Ad

Friday, May 6, 2022

MWANAMKE AFUNGWA JELA BAADA YA KUIBA MBEGU ZA KIUME ZA MPENZI WAKEMwanamke mmoja nchini Ujerumani amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kuiba mbegu za kiume za mpenzi wake.

Jaji wa mahakama ya magharibi mwa Ujerumani Astrid Salewski amesema mwanamke huyo alitoboa tundu kwenye kondomu za mwanaume huyo kwa makusudi ili apate ujauzito.

Uamuzi huo umetolewa katika mahakama ya kikanda katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Bielefeld.

Inaelezwa kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 39 alikuwa kwenye uhusiano mwanamume wa miaka 42 ambapo mwanamke huyo alimpenda sana mwanaume huyo lakini alijua kwamba mwanaume huyo hakutaka kupata naye mtoto

Mwanamke huyo alitoboa mashimo kwa siri kwenye kifurushi cha kondomu ambazo mpenzi wake alihifadhi kwenye meza yake ya kulalia kwa lengo la kupata ujauzito lakini juhusu za mwanamke huyo hazikufanikiwa

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages