MUME AMUUA MKEWE MBELE YA WATOTO, AMTOBOA MACHO NA KUMKATA SEHEMU ZA SIRI


Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Ndinyika, Kata ya Karansi wilayani Siha, Stephano Sikawa (33), kwa tuhuma ya kumchinja hadi kumuua mkewe, Sioni Daudi (26), mbele ya mwanawe mwenye umri wa miaka minne.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Simon Maigwa, amesema Sioni aliuawa na mumewe Mnamo Mei 23, 2022 akiwa nyumbani kwake kijijini huko.


"Ni kweli nimepokea taarifa kuhusu mauaji hayo ya kikatili. Mume wa marehemu imebidi tumkamate kwa sababu anahusishwa na mauaji hayo.

Amesema kuwa mtuhumiwa ametekeleza unyama huo kwa kumkata sehemu zake za siri na kuchukua kiungo hicho, akakata viganja vya mkono wa kulia, vidole viwili na kumtoboa macho mwenzi wake huyo.

Imeelezwa kuwa Kuna rekodi ya maneno yake aliyokuwa akiyasema huko nyuma kwamba atamfanya kitu kibaya.

Sasa hivi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa pamoja na Polisi Dawati la Jinsia la Wilaya na OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya) wako wanafuatilia sakata hilo," alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments