JESHI LA POLISI TANZANIA LAANZISHA KITUO MAALUMU JIJINI ARUSHA KUHUDUMIA WATALII KISHINDO CHA FILAMU YA ROYAL TOUR

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha 

Jeshi la Polisi nchini limejipanga vyema kuimarisha ulinzi na usalama baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuzindua filamu ya The Royal Tour hivi karibuni kwa lengo la kuutangaza utalii.

Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema Jeshi la Polisi Nchini limeanzisha kitengo maalumu cha Utalii na Diplomasia ambacho kipo kwa ajili ya kuwahudumia Watalii na Wanadiplomasia wanaofiika nchini.

Amesema Mkoa wa Arusha ambapo ni kitovu cha utalii nchini kumeanzishwa kituo cha Polisi maalumu kwa ajili ya kuhudumia Watalii na Wanadiplomasia ambapo Askari wake wamewapatiwa mafunzo ndani na nje ya Nchi namna bora ya kuhudumia watalii. 

Pia amesema kuwa kuna magari maalumu ambayo hutumiwa na kituo hicho kwa ajili ya doria mbalimbali ikiwemo kwenye vivutio vya utalii, hoteli za kitalii pamoja na maeneo mengine ambayo wageni hupenda kutembelea.

Sambamba na hilo amesema kuwa kuna vituo vidogo vya Polisi vilivyopo katika wiliya ya Arumeru, Monduli, Longido, na Karatu ambapo magari ya utalii hufika kwa ajili ya kupata taarifa za kitalii pamoja na ukaguzi wa usalama wa magari hayo.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi Nchini litaendelea  kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii kwa kuboresha mazingira ya kiusalama kwa watalii wanaofika nchini.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments