MAPACHA WANAOKULA MAGODORO ARUSHA KAMA CHAKULA WAOMBA MSAADA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2022

MAPACHA WANAOKULA MAGODORO ARUSHA KAMA CHAKULA WAOMBA MSAADA


Mapacha wenye umri wa miaka 9 mkoani Arusha wanaoishi huku wanakula magodoro, wanaomba msaada ili wakatibiwe.

Mama mzazi wa watoto hao, Joyce Mrema amesema tatizo lao lilianza wakiwa na umri wa miaka mitatu, ambapo walipowafikisha hospitalini madaktari walieleza kuwa hali hiyo inatokana na upungufu wa madini mwilini.

Mzazi huyo anasema kutokana na kipato chake kuwa cha chini, Joyce ameshindwa kuwahudumia watoto hao ipasavyo , ambapo yupo eneo la Sokoni One, Arusha.

Anasema awali alikuwa akiishi na baba wa watoto hao, lakini alitoweka kutokana na deni la Sh milioni tatu, hivyo kupelekwa mahakamani, ingawa hakufafanua kuhusu jambo hilo.

Amesema kutokana na hali hiyo anaomba msaada ili aweze kuwapeleka hsopitali watoto hao, waweza kupata tiba. "Kwa watakaoguswa wanaweza kuwasiliana kwa namba yangu Joyce Mrema 0763876313" amesema.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages