RAIS SAMIA AWAAPISHA MABALOZI WANNE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Balozi Macocha Mosha Tembele kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Mindi Hellen Kasiga kuwa Mkurugenzi wa Idara/Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi James Gillawa Bwana kuhudumu katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Noel Emmanuel Kaganda kuhudumia Chuo cha Ulinzi (NDC) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.

Mabalozi walioapishwa wakila Kiapo cha Uadilifu. Kutoka kulia Balozi Macocha Mosha Tembele, Balozi Mindi Hellen Kasiga, Balozi Noel Emmanuel Kaganda, Balozi James Gillawa Bwana katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Mabalozi 4 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga pamoja na Balozi Macocha Mosha Tembele, Balozi Mindi Hellen Kasiga, Balozi Noel Emmanuel Kaganda, Balozi James Gillawa Bwana katika hafla ya uapisho wa Mabalozi hao iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 April 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Donald Wright mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Donald Wright mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Donald Wright mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post