MGEJA : KINANA NI KOCHA MCHEZAJI...CCM IMELAMBA DUME


Mwenyekiti wa Shirika likisilo la Kiserikali la Mzalendo Foundation,Khamis Mgeja,amepongeza kuchaguliwa kwa Kanali Mstaafu; Abdulrahamn Kinana,kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa kudai ni chaguo sahihi kutokana na kukijua Chama.

Mgeja ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,alisema ukomavu wa Kisiasa wa Kinana na uadilifu alionao utazidi kuking'arisha Chama kiasi cha kuaminika zaidi na Wananchi kuiongoza Tanzania.

Alisema kwa Mkongwe huyo wa siasa nchini kupata wadhifa huo,atakuwa msaada mkubwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa,ambaye ana majukumu makubwa ya Serikali,hivyo Chama kitakuwa salama na kitawajibika kwa kasi na Ari mpya.

Mgeja alisema,Kinana Ni mchapakazi, mweledi, mzalendo na anarekodi ya ufanisi katika mikakati ya kisiasa na uongozi wenye matokeo chanya ambayo yalionekana katika awamu zote serikali kuanzia Serikali ya Awamu ya Nne mpaka Awamu ya Tano.
Aliendelea kusema ni kiongozi ambaye alileta uhai wa CCM.

 "Kipindi chake cha uongozi cha miaka sita kiliwafanya wana-CCM watembee kifua mbele, wakati kabla ya hapo waliona hata aibu kuvaa sare za CCM mitaani. Kinana alipambana na viongozi wa Serikali wasiotimiza wajibu wao. Niseme kwa Kinana ni Kocha Mchezaji,upele umepata mkunaji na Chama kimelamba dume kutokana na kukijua Chama,"alisema Mgeja.

Kinana alizaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha,ni msomi aliyehitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani.

Ni mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini, zikiwemo; Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

Pia amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa kipindi cha miaka 10 na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006.

Kinana aliwahi kutumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka 20 na hatimaye kustaafu kwa cheo cha ukanali.

Kinana aliteuliwa kushika ya Ukatibu Mkuu wa CCM mwaka 2012 kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Wilson Mukama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post