MDAU WA UTALII AMWAGIWA TINDIKALI


 Mdau wa utalii na mkazi wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Tariq Awadhi amedai kumwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa tindikali usoni.

Mwanaume huyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) amesema kuwa anadhani aliyemmwagia kimiminika hicho ni mtu wake wa karibu ambaye ni mwanaume.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amesema kuwa hilo linachunguzwa ili wale waliofanya tukio hilo waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

 CHANZO MWANANCHI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post