KIVULINI, POLISI MWANZA WATAKA BODABODA KUEPUKA NGONO NA WANAFUNZI, WAKE ZA WATU, KUZAA NA KUTELEKEZA

Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo jijini Mwanza.

Na Mwandishi wetu - Mwanza
Waendesha pikipiki mkoani Mwanza wametakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya uhalifu ikiwemo tabia ya kushawishi wanafunzi na kujihusisha nao kimapenzi.

Wito huo umetolewa Aprili 13,2022 na Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally wakati wa kampeni ya kuzuia na kutokomeza watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

“Ukilinganisha sababu za watoto kuwepo ama kutowepo mtaani unakuta hasara za kuwepo kwao mtaani ni nyingi mno kuliko faida, hivyo hatuna budi kama jamii mkiwemo waendesha bodaboda na makundi yote yakiwemo ya wanawake wajasiriamali,viongozi wa dini na kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu ili kufanikisha kampeni ya kuondoa watoto mtaani itakayodumu kwa muda wa wiki nane”, alisema Yassin.

Aidha Yassin aliwataka waendesha pikipiki kufanya kazi hiyo kwa malengo ili kujikomboa kiuchumi badala ya kuendekeza mambo yasiyo na tija ikiwemo ngono pamoja na ulevi wa kupindukia.

“Waendesha bodaboda mfanye kazi hii kwa faida ya familia zenu,mkumbuke kuwa ngono na ulevi hazijawahi kubadilisha maisha ya mtu ,hivyo acheni kuweka heshima baa bali wekeni heshima majumbani mwenu”,aliongeza mkurugenzi huyo wa shirika la Kivulini.

Kampeni hiyo imewafikia waendesha pikipiki kufuatia baadhi yao kunyoshewa vidole kwa kuwa chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani katika mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya waendesha pikipiki wakizungumza katika mkutano huo walikiri wengi wao kuwa na tabia ya kuwarubuni wanafunzi pamoja na kutembea na wake za watu huku wakidai baadhi yao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kushawishiwa.

“Watoto wengi wa mtaani wanatokana na sisi waendesha bodaboda kutokana na wengi wengi kuwa na tabia ya kuzaa na kisha kutelekeza,ni lazima tuambiane ukweli kama tukitaka kutibu tatizo hili”, alisema Francis John mmoja wa waendesha pikipiki katika kata ya Mirongo.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha pikipiki Kanda ya Mjini Kati Ramadhan Jacobo aliwaasa waendesha pikipiki kujiepusha na tabia ya kutongoza pamoja na kujihusisha na mapenzi na wateja wao.

“Asilimia tisini ya abiria tunaowabeba na wanaotulipa fedha ni wadada, na nyie ni mashahidi ukimpata na kumtongoza tu huyo umempoteza na akikubali umeanza kula hasara”, alisema Jacob.

Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga aliwaasa waendesha pikipiki kuzingatia sheria za usalama barabara ili kuepusha ajali zinazoepukika.

“Fuateni sheria za usalama barabarani kwa manufaa yenu wenyewe sio yangu,hakikisheni mnakuwa na helmet mimi nikikukamata huna helmet zinakutoza elfu kumi ya faini nitakuambia paki pikipiki yako hapa kituoni kanunue helmet”, alisema Fatuma.

Aidha Fatuma aliwassa waendesha pikipiki kufichua wahalifu pamoja na kutunza familia zao.

“Natambua mnafahamiana na watu wengi sana wema na wahalifu,niombe muwafichue wahalifu maanake sisi sote tunahitaji usalama. Pia tunzeni familia zenu acheni kudanganya wanafunzi kwa chipsi huku nyumbani mnaacha elfu mbili halafu unarudi nyumbani unakuta kuku na unakula bila aibu”, aliongeza Fatuma.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally (kulia) na Mkaguzi Msaidizi wa polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga wakipiga makofi wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo uliolenga kuhimiza ushiriki wao katika kampeni ya kuzuia na kutokomeza tatizo la watoto wa mitaani mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo
Mkurugenzi wa Kivulini Yassin Ally akizungumza na waendesha pikipiki kata ya Mirongo
Mkaguzi Msaidizi wa polisi kata ya Mirongo Fatuma Mpinga akizungumza na kusisitiza jambo wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo.

Wa tatu kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally akifuatilia mjadala wakati wa mkutano wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo uliolenga kuhimiza ushiriki wao katika kampeni ya kuzuia na kutokomeza tatizo la watoto wa mitaani mkoani Mwanza.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata ya Isamilo akizungumza katika mkutano wa waendesha bodaboda kata ya Mirongo kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani,kufichua wahalifu n.k
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata ya Isamilo akizungumza katika mkutano wa waendesha bodaboda kata ya Mirongo kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani,kufichua wahalifu n.k
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Waendesha pikipiki wakifuatilia mada mbalimbali
Mmoja wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo akizungumza kwenye mkutano huo
Mmoja wa waendesha pikipiki kata ya Mirongo akizungumza kwenye mkutano huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post