HATIMAYE NDUGAI AONEKANA BUNGENI


Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, (kushoto), akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga Emmanuel Cherehani wakibadilisha mawili matatu.

Baada ya kimya kirefu cha kutoonekana Bungeni, hatimaye leo Aprili 13, 2022, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ameonekana Bungeni, ambapo kiu kubwa ya Watanzania ni kutaka afunguke wapi alipokuwa ili kujibu maswali mengi ya watanzania waliyokuwa wakitaka kujua alikwenda wapi, mara baada ya kujiuzulu nafasi hiyo, na Bunge lilipoanza hakuonekana kabisa bungeni na hivyo kuleta mijadala mingi ikiwamo kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wabunge wakisalimiana na pamoja na kubadilisha mawili matatu, na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai (kushoto).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post