SIMBA SC YAZINDUA KAMPENI KUELEKEA MCHEZO WAKE DHIDI YA ORLANDO PIRATES


Afisa habari wa Simba, Ahmed Ally.

Klabu ya Simba leo Aprili 12, 2022 wamezindua kampeni ya hamasa kwa mashabiki kujitokeza kwenye mchezo dhidi ya Orlando Pirates kwenye tawi la Chang’ombe Maduka Mawili.

“Safari hii tunaenda kuandika historia ya kutinga nusu fainali. Nawaomba Wanasimba tununue tiketi mapema siku hiyo tujitokeze kwa wingi Kwa Mkapa.” amesema Afisa habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally.

“Sisi tumeshawahi kufika fainali ya michuano hii, sasa mwaka huu tunataka kwenda kushinda kombe hili. Jumapili tujitokeze kwa wingi kuliko hata Simba Day.”

“Ahmed Ally ni mtoto wa Simba, ni msemaji mwenye taaluma. Hili jambo ambalo analifanya yeye na wenzake ni kubwa sana la kuwaunganisha Wanasimba.” – Mwenyekiti wa zamani, Hassan Dalali.


“Nchi ambazo zimeingiza timu robo fainali hazizidi tano, kuna watu wanajifanya hawaoni jitihada ambazo zimefanywa na Simba. Mwakani Tanzania tutaingiza tena timu nne kwenye mashindano ya CAF na hizi ni jitihada za Simba.”

“Niwahakikishie Wanasimba na wapenzi wa soka, leo hii tunaenda kucheza mchezo kwa dakika 180 (nyumbani na ugenini) kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali sababu tuna wachezaji ambao wanajitambua, tuwaombee wafanye vizuri.”– Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post