BONDIA MWAKINYO ATOA TAMKO BAADA YA KUVULIWA TAJI LA UBINGWA ABU


Hassan Mwakinyo Bondia raia wa Tanzania akiwa ulingoni
Bondia raia wa Tanzania Hassan Mwakinyo kwa sasa yupo nchini Marekani

BONDIA Hassan Mwakinyo ametoa tamko baada ya kuvuliwa taji la ubingwa wa African Boxing Union ‘ABU’ kufuatia kushindwa kulitetea kwa muda mrefu.

Jana Jumatatu (April 11,2022), taarifa za kuvuliwa taji hilo kwa Mwakinyo zilitolewa rasmi na kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo Bondia huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani ametoa tamko lake kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuandika:

“Mkanda ni zawadi na hauna thamani ya kuuza popote kiasi mtu aone nimepata hasara sana, la hasha ila ina heshima yake kama vikombe kwenye mpira. Kuna watu wanalielezea kwa chuki na roho mbaya wakihisi naharibikiwa ila mkanda huo ni wa Afrika tu na sio dunia.

“Hata ningekuwa nao hapa nilipo leo bado usingekuwa maana kwangu kama sitapigana na wenye rank kubwa zaidi yangu. Kwa sasa focus yangu kubwa ni kupata nafasi ya kucheza mikanda mikubwa ya nafasi ninazo tamani kufika kidunia,” amesema Mwakinyo.


Wakati huo huo Rais wa African Boxing Union (ABU), Houcine Houichi amesema kwamba bondia Hassan Mwakinyo alipewa ofa ya Dola za Marekani 20,000 (Tsh Mil 46) ili kuutetea ubingwa wake dhidi ya bondia kutoka Afrika Kusini, Brendan Thysse, lakini alikataa na kutaka apewe Dola 40,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post