MISA TAN YAENDESHA MAFUNZO YA SHERIA ZA VYOMBO VYA HABARI KWA WANACHUO WA SJMC - UDSM


Mkufunzi, Bi. Salome Kitomari akiendesha mafunzo kuhusu Maadili ya uandishi wa habari kwa wanachuo wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Afisa Habari na Utafiti wa MISA TAN, Bi. Neema Kasabuliro akizungumza na wanachuo wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaoshiriki wa mafunzo ya siku 2 ya Sheria za vyombo vya habari nchini.
Mkufunzi, Wakili James Marenga akiendesha mafunzo kuhusu sheria za vyombo vya habari kwa wanachuo wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Wanafunzi wa Uandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya Sheria za vyombo vya habari yanayoendelea katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC)

Wanafunzi wa Uandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya Sheria za vyombo vya habari yanayoendelea katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC).
 ****

Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na taasisi ya sheria ya Marekani (ABA ROLI) inaendesha mafunzo ya sheria za vyombo vya habari nchini kwa wanachuo wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


Mafunzo haya ya siku mbili yanayofanyika chuoni hapo kwa kuwahusisha wanachuo wa shahada ya kwanza katika fani za Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa ABA ROLI wa Kuhimiza Uhuru wa Kutoa Maoni nchini Tanzania na Uganda.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa Habari na Utafiti wa MISA TAN, Bi. Neema Kasabuliro alieleza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Taasisi hiyo wa kukiaandaa vyema kizazi kijacho cha Wanahabari ili kuzielewa, kuzitafsiri na kuzitumia ipasavyo sheria mbalimbali zinazoongoza tasnia ya uandishi wa habari na mawasiliano hapa nchini Tanzania. 


Mafunzo haya ni muendelezo wa utekelezaji wa majukumu makuu ya MISA TAN ya kutetea, kuhimiza na kulinda uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari, na haki ya raia kupata taarifa.


 “Tokea kuanzishwa kwake MISA TAN imekuwa ikifanya kazi za uraghibishi na kuendesha kampeni mbalimbali zinazolenga kuboresha sera na sheria zinazofifisha haki ya kikatiba ya kupata na kutoa taarifa. Aidha, tunafanya tafiti kuhusu utekelezaji wa sheria hizo, hali ya uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na kufuatilia matukio ya uvunjaji wa haki tajwa hususan dhidi ya Wanahabari”, alifafanua.

Katika mafunzo haya washiriki wataweza kuongeza maarifa na uelewa wa sheria hizi na kanuni zake, vikwazo na vitisho dhidi ya uhuru wa kujieleza, pamoja na kuzitumia katika utekelezaji wa kazi za uandishi wa habari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments