INSTAGRAM YAZIMWA URUSI


Watumiaji wa mtandao wa Instagram nchini Urusi wamepewa taarifa kuwa huduma hiyo imesitishwa kuanzia saa sita usiku Jumapili ya March 14 2022 baada ya Mmiliki wake Meta Platforms kutangaza wiki iliyopita kuwa itawaruhusu Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Ukraine kutuma ujumbe wakushinikiza Wavamizi wakirusi wauawe.

Emails kutoka kwa Mdhibiti wa Mawasiliano wa Serikali ya Urusi iliwataka Watumiaji kuhamisha picha na video zao kutoka kwenye mtandao huo wa Instagram kabla ya kuzimwa ikiwa ni siku 2 baada ya Kampuni ya Meta ambayo pia inamiliki Facebook (FB) kusema mabadiliko ya muda mfupi katika sera yake ya matamshi ya chuki yanahusu Ukraine pekee kufuatia uvamizi wa Urusi wa Februari 24.

Kampuni hiyo ilisema itakuwa vibaya kuwazuia Waukraine kuonyesha hisia zao na hasira kwa vikosi vya kijeshi vinavyoivamia, kauli ambayo ilipokelewa kwa hasira na Serikali ya Urusi na kuifanya kufungua uchunguzi wa jinai dhidi ya Kampuni ya Meta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post