WANAOVUNA MCHANGA HOLELA ZANZIBAR WAONYWA


Naibu wa Waziri wa Maji ,Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaaban Ali Othman

Na Doreen Aloyce, Zanzibar

Naibu wa Waziri wa Maji ,Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaaban Ali Othman ametoa onyo kali kwa yeyote atakayekiuka sheria za uvunaji wa Rasilimali za nchi hususani mchanga atachukuliwa hatua ikiwemo kuwajibishwa bila kujali cheo chake.


Kauli hiyo aliitoa jana kwenye semina elekezi kwa wakuu wa Wilaya ,maafsa wa maliasili lengo Likiwa ni kukumbushana na kujenga uelewa wa pamoja kuhusiana na masuala ya sheria ambazo zinatumika katika kudhibiti na kuratibu masuala ya maliasili.


Pia ametahadharisha baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo ambao wanahusika kujua wanaofanya vitendo hivyo vya uvunaji holela wa Rasilimali na kunyamaza jambo ambalo halitafumbiwa macho.

Amesema semina hiyo ni baada ya kubaini kuwa kuna uelewa tofauti kwenye maeneo yale ya kiutawala hasa Wizara inapopanga taratibu zake na utekelezaji haufanikiwa kadri ilivyokusudia.

Aidha amesema kutokana na kinachoendelea hasa cha uvunjifu na ukiukwaji wa taratibu katika maeneo yao hasa uvunaji wa Rasilimali Mchanga wakaona ni vyema wakae pamoja ili wawe na mwelekeo wa mmoja namna ya kudhibiti Rasilimali hizo .

Amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa ambapo fedha nyingi za Serikali zinapotea kutokana na mashimo mengi ambayo sio rasmi na wasafirishaji,wanunuzi ambao hawako kwenye mfumo.

"Wizara tumejipanga kusimamia hilo hatutamfumbia macho atakayebainika kuvunja sheria niwaombe warudi katika mfumo ambao umewekwa kisheria na sio vinginevyo lengo ni kuvuna na kuratibu na hatimaye kuwa na uelekeo mmoja kama Serikali",amesema.


"Nakuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara kuhakikisha kamati zitakazoundwa na wakuu wa Wilaya yao watakaounda kamati za kutusaidia sisi kukamata Rasilimali hizo na kuletwa hapa wizarani na wale kupigwa faini wapewa asilimia ili kuweka motisha kwao kutokana na gharama walizozitumia",amesema.

Kwa upande wao wakuu wa Wilaya walíiopata semina hiyo wamesema itaenda kuleta tija kuokoa Rasilimali za nchi na kwamba wananchi watambue kuwa Zanzibar ni ndogo kama watachimba bila mpangilio itakuwa hasara kwa Taifa na vizazi vijavyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments