DC SERENGETI: RUWASA WAIMARISHE MIUNDOMBINU YA MAJI


Afisa Utumishi RUWASA mkoa wa Mara,Stanley Sing'ira akifungua bomba la maji lililopo kijiji cha Makundusi kata ya Nata -Serengeti
Mradi wa Maji kijiji cha Makundusi Kata ya Nata
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt.Vicent Mashinji


Meneja RUWASA wilaya ya Serengeti Deus Mchele


Na Dinna Maningo, Serengeti
Mkuu wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Dkt.Vicent Mashinji ameitaka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhimarisha miundombinu ya maji kwani baadhi ya miradi wakandarasi hufanya vibaya nakusababisha kuwepo kwa dosari kwenye miradi ya maji.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake,mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kuna udhaifu kwa baadhi ya wakandarasi wanaofanya kazi ya kujenga miradi ya maji na kusababisha miradi kuwa chini ya viwango vinavyotakiwa.

"RUWASA wahimarishe Miundombinu ya maji kuna udhaifu kwa baadhi ya wakandarasi wanaofanya kazi aidha hawana ujuzi na kazi ama wanabana matumizi ili wapate faida kubwa ya pesa,kuna miradi mitatu ilileta shida ya kutopatikana kwa maji", alisema Mashinji.

Mashinji aliongeza kuwa kuna changamoto ya umeme,baadhi ya miradi ya maji ilipojengwa hakuna umeme inaendeshwa kwakutumia mionzi ya jua (Sola),na kwamba kuna maeneo mengine ili kufikisha umeme kuliko na mradi wa maji zinahitajika nguzo 10.

"Bado kuna changamoto ya umeme kwenye baadhi ya miradi,tunamshukuru Rais wetu mama Samia kutupatia fedha za miradi ya maji tunamuomba pale tunapokwama asisite kutusaidia,maendeleo lazima yawepo maana watu wanaongezeka na matumizi ya maji yanaongezeka na lengo letu kubwa ni kupata maji kutoka ziwa Victoria",alisema.

Mkuu huyo aliipongeza RUWASA kuwa imekuwa ikijitahidi kuwafikia wananchi kwa kujenga miradi ya maji na miradi mingine kukarabatiwa nakwamba upatikanaji wa maji katika senta ya Serengeti umeongezeka.

" Tatizo lililopo wananchi wetu baadhi hawapendi kukaa kwenye senta wanakaa mbalimbali sana wana mifugo kila mtu anataka akae peke yake kwahiyo usambazaji wa maji unakuwa shida.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Deus Mchele alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022,serikali imetenga fedha Bilioni 6.2 kujenga miradi ya maji vijiji 20 kwenye wilaya hiyo ambapo tayali wamepokea fedha Bilioni 3.2.

Mchele alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kujenga miradi mitano mipya ya maji,kukarabati miradi 10 ya maji na mitano kufanyiwa upanuzi nakwamba miradi yote itakamilika ifikapo juni,30,2022.

Mkazi wa kijiji cha Makundusi kata ya Nata,Mwajuma Magige alisema kuwa kijiji hicho kimepata mradi wa maji na wananchi wanapata maji nakwamba kabla ya mradi huo waliteseka kupata huduma ya maji iliyowaradhimu kutembea umbali mrefu kufuata maji mtoni.

"Tunashukuru Rais wetu kwakutujali sisi akina mama tulikuwa tunateseka maji unatembea masaa mawili ,ukiwa njiani lazima utue maji chini upunzike mara tatu njiani ndiyo ufike nyumbani,wajawazito walipata shida kwa siku huwezi kufuata maji zaidi ya ndoo mbili,maji yalitufanya tuwe wachafu mpaka tulitengwa hata kwenye sherehe kuwa wanawake wa Makundusi ni wachafu",alisema Mwajuma.

Mwenyekiti wa kijiji cha Makundusi Josephu Mseti alisema kuwa mradi huo utawasaidia wananchi kuwapunguzia mwendo zaidi ya km 4 kuyafuata mtoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments