WAENDESHA BODABODA, BAJAJI NA WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII 'NSSF'


Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewashauri Waendesha bodaboda,bajaji na Wajasiriamali wajiunge na kujiwekea akiba kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadae, kutimiza malengo yao na kuweza kupata Pensheni ya uzeeni.

Rai hiyo imetolewa Februari 9,2022 na Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance wakati akitoa elimu kwa waendesha bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi pamoja na fursa zinazotolewa na taasisi mbalimbali ikiwemo NSSF.


Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance alisema NSSF imefungua milango kwa ajili ya Wajasiriamali, wakulima,wavuvi na watu wote waliojiajiri wenyewe hivyo kuwaomba wajiunge na NSSF ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo na kujiwekea akiba ya baadae.

"Mjasiriamali, mkulima,mvuvi na wote waliojiajiri wenyewe NSSF imewafikia, njoo ujiunge na ujiwekee akiba kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadae, kutimiza malengo yako na pia kuweza kupata pension ya uzeeni",alisema Janeth.

"Pia kwa wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vya kati kuna fursa ya mikopo ambayo mikopo hii inalenga kuchochea kukua na kuongezeka kwa viwanda vya ndani. Mikopo hii itawasaidia kukuza mtaji ,kununua malighafi na kununua mashine na vitu vitakavyotumika katika uzalishaji kwenye viwanda husika",alieleza.


Alifafanua kuwa Mikopo hii inatolewa kwa ushirikiano kati ya NSSF,SIDO,VETA, NEEC na AZANIA Bank.,Mwanachama anaweza kunufaika na mkopo huo kuanzia shilingi 8,000,000/= mpaka shilingi 500,000,000/= kulingana na uhitaji nawa uwezo wake wa kurudisha mkopo, Marejesho ya mkopo huu ni kuanzia mwaka 1 mpaka 7 kulingana na kiwango huku riba yake ikiwa 13%.


"Ikumbukwe kuwa kujiunga na NSSF ni bure ambapo Kima cha chini cha kujichangia kwa mwezi ni shilingi 20,000/= au zaidi kulingana na kipato. Mwanachama anaweza kuweka mara moja kwa mkupuo au kuweka kidogokidogo kila siku au kila wiki ili kufikia au kuzidi kiwango hicho kulingana na malengo au kipato cha mwanachama",alieleza Janeth.


"Kutolewa kwa mikopo yote hii hakuta angalia kiasi mwanachama alicho jihifadhia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF. Mwanachama anaweza kujichangia pindi atakapopata control namba yake(kumbukumbu namba) kwa watoa huduma wote wa fedha kama Mpesa, Tigo pesa, Airtel Money, Halo pesa pia kwa Mawakala wote wa huduma za Benki",aliongeza.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga Jumatano Februari 9,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde  1 blog
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga wakifuatilia elimu iliyokuwa inatolewa
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance (katikati) akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post